Makusudi ya Mungu ni kuwafikia wanadamu waliopotea. Kwa njia gani?

Ezekieli 47:1-12: Picha aliyoonyeshwa Ezekieli ni ya Hekalu la Mungu na mto unaotoka katika hekalu hilo. Mungu aliongea na Ezekieli na kumwonyesha kwamba huu ulikuwa Mto wa Uzima unaotiririka kutoka kwa Mungu hadi kwenye bahari ya chumvi na kuingia katika maji machafu yaliyooza. Mto huu utayaponya maji hayo na kuyafanya hai.

Kwa kawaida bahari katika Biblia, humaanisha bahari ya wanadamu waliopotea. Mungu alikuwa akimuonyesha Ezekieli kwamba njia pekee ya kuwafanya wanadamu waweze kuishi, ni kwa kuguswa na Mungu, kwa njia ya kitu kinachoitwa Mto unaotiririka kutoka katika uwepo wake mwenyewe.

Katika Yohana 7:38 imeandikwa hivi, “Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, Mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.”

Maadui zetu huja kwetu kwa njia kuu tatu

Katika Luka 9:23-25 Biblia inasema, “Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha. Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza, au kujipoteza mwenyewe?

Neno hilo nafsi katika Luka 9 linamaanisha utashi, akili na hisia. Neno kukana linamaanisha kukataa kitu fulani.

Ufunguo wa kupata uzima tele na kupokea baraka kutoka kwa Yesu, hii ikiwa ni pamoja na uwepo wake, ni kukamilisha agano la damu kwa kubeba msalaba wetu.

Wengi wetu tunajua kazi nzuri sana, yenye uweza mkuu, iliyohusisha kila kitu, ambayo Yesu aliifanya juu ya msalaba wa Kalivari, jinsi alivyomwaga damu yake kwa ajili ya dhambi zetu, na kufufuka katika wafu ili kutupatia uzima. Hatuwezi kuongeza chochote juu ya hayo. Hata hivyo, ili tuweze kunufaika na kazi hiyo, hatuna budi pia kufa. Lazima tubebe msalaba wetu, tujikane wenyewe na kumfuata. Ni lazima tuiangamize nafsi yetu.

Uhusiano na USHIRIKA wetu na Mungu umejengwa juu ya msingi wa agano la damu. Kwa wengine jambo hilo linaweza kuonekana geni. Jambo hilo linaweza kulinganishwa vizuri zaidi na ndoa. Watu wengi sana wana ufahamu usio wa kibiblia kuhusu uhusiano huu wa agano la damu. Hebu jiulize swali hili: Je, ungeweza kujadiliana na mchumba wako kuhusu uhusiano mwingine wa kimwili unaoruhusiwa kuwa nao na wanawake wengine baada ya ndoa?

Ni kitu gani muhimu sana kuhusu agano la damu?

Katika kitabu cha 1 Petro 1:18-19 tunasoma maneno yafuatayo: “Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.”

Katika Mambo ya Walawi 17:11 tunasoma pia maneno yafuatayo: “Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi.”

Maisha ya kiroho yanaweza kubadilishana na ile sheria ya mbadala. Agano la damu hubadilisha urithi wa familia yako.

Kimsingi, hii ina maana kwamba watu wanaweza kuzaliwa katika familia fulani, na katika familia au ukoo wao huo, wakapokea baraka na laana kama urithi wao. Hata hivyo, baraka na laana zinaweza kubadilishwa. Makabila kadhaa katika bara la Afrika, na pia katika utamaduni wa Wahindi wekundu na katika jamii nyingine za Asia, yamekuwa kila wakati yakitafuta njia za kubadilishana na watu wengine baraka na laana.

Kabla ya kuumbwa kwa dunia, Mungu alikuwa amepanga kwamba Yesu asulibiwe kulingana na Roho wa UZIMA, na hii ina maana kwamba ile kanuni ya mbadala ilikuwa ikitenda kazi hata kabla mwanadamu hajaumbwa (Ufunuo 13:8).

Ili agano la damu liweze kweli kufanya kazi, ni lazima kila upande unaohusika umwage damu, au ni lazima viwepo vifo viwili au misalaba miwili. Lazima utu wetu wa kale ufe na kisha tujikabidhi sisi wenyewe na vyote tulivyo navyo kwa Yesu. Jambo la kufurahisha ni kwamba hata Yesu mwenyewe ametoa yote aliyo nayo na kujitoa mwenyewe kwetu!

Kila wakati kunakuwa na misalaba miwili inayopaswa kuungana ili kufanya agano la damu.

Hema ni alama yenye nguvu ya misalaba miwili inayofaa kutumiwa kama mwongozo wa maombi. Itatusaidia kubeba msalaba wetu na kutuingiza katika uwepo hasa wa Mungu na kuwa na USHIRIKA naye!
"Agano la Kale linatuambia jinsi wateule wa Mungu walivyoishi duniani. Kwanza, Hema lilitumika kama kituo cha makabila 12; baadaye Hekalu ndilo lililokuwa kituo chao. Kituo cha Hekalu kilikuwa Sanduku. Hema, Hekalu na Sanduku ni aina mbalimbali za Kristo. Kadri wana wa Israeli walivyokuwa na uhusiano mzuri na Hema au Hekalu walipata ushindi, na hakuna taifa lililoweza kuwashinda. Ingawa wana wa Israeli walikuwa hawajui kupigana, waliwashinda maadui zao wote waliokuwa wamejifunza jinsi ya kupigana. Lakini wakati walipokuwa na tatizo kuhusiana na Hema au Hekalu, walichukuliwa utumwani. Haikusaidia kitu kuwa na wafalme wenye nguvu au hekima kubwa, kitu muhimu kilichoangaliwa ni iwapo wamelikosea sanduku la maskani au hekalu. Walipotoa kipaumbele kwa Mungu, ushindi ulikuwa wao. Ndivyo ilivyo hata leo. Tukiuzingatia ushindi wa Kristo, sisi pia tutapata ushindi." Dondoo kutoka katika kitabu kiitwacho "God's plan and the Overcomers" (Mpango wa Mungu na washindaji), kilichoandikwa na Watchman Nee
Unavyoendelea kuwa na ushirika na Mungu, jaribu kujiona kana kwamba unatembea katika Hema kama jinsi makuhani wa Agano la Kale walivyofanya.

Tunaanzia hapa Tunatembea mpaka hapa Tunaishia hapa na kubeba msalaba wetu katika uwepo wa Mungu

Hema

Ua wa nje Patakatifu

Patakatifu pa Patakatifu Beba msalaba wako Mahali tunapokutana na Mungu

Nia (Akili)

Madhabahu ya kufukizia

Hisia

Wonyesho

Utashi

Mapazia

Kwanza: Msalaba Wake Kwanza: Msalaba Wake

Kwa ajili yako

Nyakati za Agano la Kale, kila mwaka Wana wa Israeli walikuwa wakiadhimisha Siku ya Upatanisho ijulikanayo kama "Yom Kippur". Dhambi za wana wa Israeli zilikuwa zikishughulikiwa katika siku hii moja tu ya mwaka, wakati kuhani mkuu alipojiandaa kuingia katika Hema kwa niaba ya wana wa Israeli kwa ajili ya dhambi zao.

Pale kwenye madhabahu ya Shaba, katika ua wa nje, kulikuwa na mbuzi wawili. Mmoja alifungwa kitambaa chekundu shingoni mwake kuonyesha kwamba atachinjwa kwa ajili ya damu. Mwingine alifungwa nje ya lango kuonyesha kwamba angekuwa Azazeli. Mbuzi wa kwanza alichinjwa madhabahuni na damu yake ilipelekwa na kuhani patakatifu pa patakatifu ambapo aliitoa kwa kufukizia kando ya madhabahu ya kufukizia (mahali pa sifa). Uvumba ulipokuwa ukiungua, ulisababisha moshi ujae patakatifu pa patakatifu, na hiyo iliwakilisha (na kuleta hasa) uwepo wa Mungu. Kuhani alinyunyiza damu juu ya Kiti cha rehema mara moja na pia alinyunyiza damu mbele ya Kiti hicho mara saba. Nje ya marago, kila mtu alilala kifudifudi wakati yote hayo yalipokuwa yakiendelea. Hakuna mtu aliyeona chochote kilichokuwa kikifanyika, na hiyo ilimaanisha kwamba dhambi zao zilisamehewa kwa mwaka mzima.

Pili, kuhani aliporudi na kubadili nguo zake, aliweka mikono yake juu ya mbuzi mwingine, Azazeli, kuashiria kwamba dhambi zote zimehamishiwa juu ya kichwa cha mnyama huyo. Kulikuwa na mtu aliyechaguliwa kumpeleka mbuzi huyo jangwani mahali pasipokaliwa na watu na kumwacha sehemu ambayo hawezi tena kurudi au kutoroka. Mtu huyo kwa mfano, alimpeleka mbuzi yule hadi kwenye bonde lililozungukwa na miamba na majabali na kisha mbuzi yule aliteremshwa chini ili asiweze kutoroka(Mambo ya Walawi 16:21-22).

Sasa kuhani alipoweka mikono yake juu ya mbuzi aliye hai, ili kuanza sehemu ya pili ya ibada, aliungama dhambi zote za wana wa Israeli. Alisema, “Bwana, weka dhambi zangu na za wana wa Israeli juu ya kichwa cha mbuzi huyu. Haya, we mbuzi, ondoka." Mbuzi yule alipokuwa akipelekwa nje ya marago, watu wote walisimama na kushangilia. Watu wote na hata watoto waliweza kuona tukio hilo na kufahamu. Azazeli ni mfano wa Yesu aliye Azazeli wetu, aliyeshushwa chini hata kuzimu kwa ajili yetu huku dhambi zetu zikiwa juu ya kichwa chake. Alichukua dhambi zetu na kuziondoa kabisa, zisionekane tena au kurudi. Zaburi ya 103:12 inasema "Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao." Katika kitabu cha Mika 7:19 tunasoma pia maneno haya "Atarejea na kutuhurumia; atayakanyaga maovu yetu; nawe utazitupa dhambi zao zote katika vilindi vya bahari."

Katika kitabu cha Waebrania 9:12-14 tunapata pia maneno yafuatayo "wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng'ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kutusafisha mwili; basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?"

Hema

Ua wa nje Patakatifu

Patakatifu pa Patakatifu Beba msalaba wako

Mahali tunapokutana na Mungu katika uwepo wake

"Mto Utiririkao" (Mwongozo wa Maombi ya Kila Siku)

Kusafiri hadi katika Uwepo wa Mungu

Maelekezo:

  1. Soma kwanza kurasa 7 za mwanzo, na kisha zisome tena angalau mara moja kwa mwezi. Halafu kila siku, anzia ukurasa huu, na uwe na muda wa kuwasiliana na Mungu angalau kwa dakika ishirini.
  2. Utakapoanza na hema ya kukutania, mgongo wako unapaswa kuielekea dunia huku uso wako ukimwelekea Yesu. Hii ni muhimu kwa sababu Roho Mtakatifu hawezi kukaa na wewe iwapo unaelekea mahali pabaya. (mwelekeo wa kiroho, Matendo ya Mitume 26:18)
  3. Nenda hadi kwenye kila “kituo” ushughulike na somo hilo katika hali ya maombi pamoja na Bwana. Tafuta katika Biblia baadhi ya maandiko. Uwe macho kuhusu maeneo yanayohitaji toba, kwa sababu jambo hili ni moja kati ya michango yetu mikubwa, wakati huu tunapokuwa na ushirika na Mungu.
  4. Ni vema ukipitia vituo hivi vyote kwa wakati mmoja. Unaweza kufanya hivyo kwa DAKIKA ISHIRINI. Hata hivyo, kama huna muda wa kupitia utaratibu huu wote kwa mkao mmoja, usikate tamaa. Badala yake, anza utaratibu huu asubuhi, na umalize angalau hatua moja. Kisha endelea na hatua ya pili wakati wa chakula cha mchana. Kama unahitaji, endelea siku inayofuata. Hatimaye ishi maisha yanayofuata utaratibu huu na itakuwa kawaida kwako kukaa katika uwepo wake Mungu.

Ua wa Nje

Kituo cha kwanza: Madhabahu ya Shaba - Msalaba wa Yesu. Msamaha

yote aliyo nayo Mungu. Hata hivyo hatuwezi kupata msamaha wa dhambi bila kumfanyaYesu kuwa Bwana (Warumi 10:9-10).

Anza leo kuwa mkweli mbele za Yesu. Neno la Mungu katika 1 Yohana 1:9 linasema "Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote."

Sehemu kubwa ya kubeba msalaba wako ni kuwa MKWELI KABISA mbele za Mungu. Unahitaji kuwa wazi kabisa na kumwambia kila kitu. Uwe na muda wa kuumimina moyo wako kwa Mungu kama jinsi ambavyo ungefanya kwa mtu ambaye ni rafiki yako sana! Biblia inasema katika 1 Yohana 1:7 kwamba "tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote." Yesu alisema katika Yohana

3:19 kwamba dhambi haina nguvu iwapo watu watakuja kwenye nuru pamoja na kweli, bila kujaribu kujificha gizani. Yesu hakufa kwa ajili ya visingizio vyetu. Alikufa kwa ajili ya dhambi zetu!

Unahitaji kutembea katika upendo, na ikitokea kwamba umefanya dhambi, kimbilia kwa Mungu, usafishwe.

"Sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti"(Warumi 8:2). Tukimgeukia Mungu kila wakati, na kudumu katika hali ya uaminifu mbele zake, atatushindia makosa yetu na vikwazo.

Angalia Mto Utiririkao Kiambatisho cha F ujitathmini mwenyewe kwa uaminifu. Kama hakuna dhambi zinazojulikana, basi kiri kwa kinywa chako maneno yaliyoandikwa katika Wagalatia 2:20 na 2Wakorintho 5:21.

Kwa kuwa sasa fahamu zetu ziko wazi na tunaweza kuwasiliana na

Mungu, hebu twende kwenye Neno. Neno linasema kwamba kuhani angekufa kama angejaribu kuingia patakatifu kabla ya kusimama kwenye birika. Hatuwezi kwenda katika uwepo wa Mungu bila kusafishwa na Neno la Mungu (Waefeso 5:26-27).

Birika litatuondolea uchafu wa dunia. Litakuwa pia kioo cha kutuhukumu, litatuletea katika akili zetu mambo tunayopaswa kurekebisha mbele za Mungu. Neno litahuisha nafsi zetu ili tuweze kufikiri kiroho na kuwa kinyume na maneno ya pepo yanayokuja katika akili au fahamu zetu.

Neno linatuambia pia kwamba Shetani amekwisha hukumiwa (Yohana 16:11). Hakikisha unasema maneno haya kwa sauti "Shetani umekwisha hukumiwa, umeshindwa!"

Tumia dakika chache katika Neno!

a. Tumia kitabu chako cha sala

b.
Tumia kitabu chako cha "ISOB" au kitabu kingine cha kujifunzia Biblia.
c.
Soma kitabu cha Mithali
d.
Soma Zaburi sura moja au zaidi.
e.
Soma vitabu vingine vinavyohusu Biblia au soma tu Biblia na umwombe Roho Mtakatifu akutafsirie. Soma Biblia yote kwa mwaka mmoja.

f. Sikiliza mafundisho au kanda za nyimbo zenye Neno la Mungu.

Kituo cha Tatu: Pazia la Kwanza: Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; nyuani mwake kwa kusifu.

Kwa kuwa sasa umekaa katika Neno, unajua uko safi mbele za Mungu na kwamba Shetani amehukumiwa, basi unayo mengi ya kumshukuru Mungu! Hata kama huoni kwa haraka mambo ya kumshukuru Mungu jaribu kuyatafuta. Kama umeshindwa kuyapata, mshukuru kwa Neno lake linalosema kwamba unao ushindi ukiendelea kulishikilia Neno. Mshukuru pia Mungu kwa ahadi alizokuahidi ambazo bado hazijatimia

katika maisha yako.

Kituo kinachofuata kipo ndani ya Patakatifu Hapa ndipo unapompa Yesu utashi au mapenzi yako na Yeye

anakuonyesha mapenzi yake, unampa ufahamu wako na Yeye anakupa ufahamu wake, unampa hisia zako na Yeye anakupa hisia zake. Huku ndiko kuubeba msalaba wako, kujikana mwenyewe na kumfuata Yesu (Luka 9:23)

Badilisha haja za moyo wako (hata kama ni nzuri) kwa ajili ya mpango au mapenzi ya Mungu katika maisha yako. Weka chini matakwa na mipango yako na umwombe Mungu akuonyeshe mapenzi yake na mipango yake kwako.

Kila wakati Mungu huangalia utashi au mapenzi yetu; hii ndio maana ya mkate wa wonyesho. Mkate ni unga uliosagwa, ukachanganywa na mafuta na kuokwa motoni. Matakwa yetu na hamu zetu ni lazima kila wakati zitolewe madhabahuni zisagwe na kuchomwa. Hii ni sadaka maalum kabisa kwa Mungu, kwa kuwa ni utashi wetu, na yeye hawezi kutulazimisha wala kutuamrisha kufanya hivyo. Itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu (Warumi 12:1-2).

Amua kusamehe hata kama hujisikii kufanya hivyo. Hii ni nafasi ya kutubu na kuacha njia za kidunia na kuzifuata njia za Mungu. Tunapoacha njia mbaya, tunapata nguvu za Mungu (Mdo 26:18 na 2 Kor 3:16).

Badilisha tamaa za mwili, uwe na tunda la Roho. Tunda la Roho ni: upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi (Wagalatia 5:19-23).

Badili nia au mawazo yako ya zamani uwe na nia ya Kristo. Katika 2 Kor 10:4-6 tunaambiwa kwamba vita viko katika mawazo na fikra zetu. Na kwamba ngome ni mawazo yetu. Mawazo haya hutufanya tuwe mbali na elimu ya Mungu. Kuna mengi ya kusema hapa kwa sababu mawazo yetu ni sehemu muhimu ya maisha yetu. Tunapaswa kuyaweka huru mawazo yetu. Kwa njia gani? Tulipokuwa watumwa wa dhambi tulitumia Mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya ambao ni mawazo yetu. Sasa tunapaswa kutumia Mti wa Uzima ambao ni Neno la Mungu. Siwazi tena na kuamua, bali natumia akili zangu kwa sababu ni makusudi ya Mungu, na hiyo ndiyo kusikia na kutii! Hii pekee ndiyo itakayoangusha ngome katika akili zetu. Tukiuona utukufu wa Mungu kama Paulo alivyouona alipokuwa njiani kuelekea Dameski, hatuwazi tena, tunasema tu, “Bwana, unahitaji nifanye nini.”

Mara kwa mara pepo hutushitaki na kushambulia akili zetu kwa kutumia nusu ukweli. Katika Isaya sura ya 11 tunaambiwa kwamba Mungu hubadilisha maarifa yetu ya asili na kutuwekea yale ya Roho Mtakatifu, yaani Roho wa Bwana, hekima na ufahamu, shauri na uweza, maarifa na kumcha Bwana.

Tunahitaji mawazo au nia zetu zifanywe upya kwa Roho Mtakatifu na Neno la Mungu (Warumi 12:2). Wakati mwingine hatujui kuomba jinsi itupasavyo. Katika Warumi 8:26 tunaambiwa kwamba tukiomba kwa lugha, tutaomba sawa sawa na mapenzi kamili ya Mungu. Kwa hiyo kila unapoomba kwa lugha utakuwa unaomba sawa sawa na Neno la Mungu na pia sawa sawa na mapenzi ya Mungu. Ile sehemu inayohusika na usemi au kunena, hutawala akili, na hivyo nia au mawazo yako hufanywa upya na kusawazishwa ili yaweze kuuambia

Badilisha hisia zako za zamani zilizosababishwa na mwili wako na ulimwengu, na nafasi yake ichukuliwe na tunda la amani, furaha, upendo, tumaini, nk. Hapa ni mahali pa dhabihu za sifa. Soma Zaburi 145-150 kwa sauti kubwa, kama hujisikii kumsifu Mungu moyoni mwako. Mungu anawatafuta watu wanaomwabudu katika Roho na kweli (Yohana 4:24). Kutoka katika mahali hapa pa sifa, Mungu atakutafuta na atahitaji kuwa pamoja nawe!

Mpatie hizo hisia ambazo umekuwa ukificha; labda ni machozi yako, labda ni kuinua kwako mikono, au labda ni kumfunulia tu hisia zako za kweli. Songa mbele, hakuna mwingine anayeangalia isipokuwa Yeye!

Mbele ya madhabahu hii kuna pazia linaloficha au kutenganisha patakatifu pa patakatifu na uwepo wa Mungu. Mungu anataka upite katika pazia hilo mara nyingi zaidi ya vile unavyohitaji. Atakusaidia kufanya hivyo. Hakuna mwanadamu wa kawaida anayeweza kuingia hapo bila kufa.

Pazia hili lilipasuka kutoka juu hata chini wakati Yesu alipokufa msalabani, akatuwezesha kuingia katika uwepo wa Mungu kwa damu yake, na kuonyesha kwamba kifo chake kimeondoa kizuizi kilichosababishwa na dhambi. Kizuizi hicho kilikuwa kinatuzuia kuingia katika uwepo wa Mungu. Msifu Mungu kwa ukweli huu.

Patakatifu pa patakatifu ni mahali aambapo hakuna mwanga au taa isipokuwa kwa ajili ya Mungu. Kuhani Mkuu aliweza tu kuingia hapa mara moja kwa mwaka, tena kwa masharti maalum. Ukweli ni kwamba madhabahu hii iliingia Patakatifu pa Patakatifu pamoja na Kuhani Mkuu mara moja kwa mwaka. Hii inaashiria kwamba kusifu kwako na kuabudu hakuishii hapa bali ni mlango wa kuingia katika uwepo wake, na mambo hayo huenda pamoja nasi.

Hili hapa Sanduku la Agano. Limefunikwa na Kiti cha rehema kilichonyunyiziwa damu. Tulihitaji rehema kwenye madhabahu ya shaba, yaani msalaba, mwanzoni kabisa. Lakini sasa katika uwepo wake kuna ufahamu mkubwa wa rehema yake na damu ya Yesu kwa namna ambayo Roho Mtakatifu pekee ndiye awezaye kukuonyesha. Rehema zake ni za milele. Ni kama haiwezekani kabisa kuandika rehema zake jinsi zilivyo, ni lazima mtu apate uzoefu wa rehema hizo.

Katika kila upande kuna malaika wakubwa wanaolinda kila kitu. Hapa pia hakuna nuru kabisa au taa isipokuwa kwa ajili ya Nuru ya Mungu.

Kumbuka, sanduku la agano lipo sasa ndani ya mioyo yetu! Sio tena kitu cha nje. Sisi ni hekalu la Mungu. Tafakari jambo hilo."Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?" (1 Kor 3:16).

Yaliyomo katika Sanduku la Agano yanaashiria mambo makubwa matatu

Mana au Neno la Mungu: Unapokuwa katika uwepo wa Mungu, Neno la Mungu lililofunuliwa huwa hai! Kama unao muda, hapa ni mahali pazuri sana pa kufungua Biblia yako na kumruhusu Bwana aseme nawe.

Mbao za sheria: Huu ni ukumbusho wa thamani kwamba sheria ya Mungu imeandikwa katika mioyo yetu. Siyo tena orodha ya mambo tunayopaswa kufanya au kutofanya.

Fimbo ya Haruni: Hii inamaanisha huduma yetu iliyopakwa mafuta ya kuwa watendakazi na mashujaa wa maombi kwa ajili ya Mungu. Kulikuwa na fimbo 12 zilizovunjika za mti wa mlozi zilizowekwa Hekaluni kwa amri ya Mungu. Fimbo mojawapo ambayo ingechipua kimiujiza wakati wa usiku, ingekuwa ile ambayo mmiliki wake ni mhudumu aliyechaguliwa na Mungu. Ni Mungu pekee anayetupatia huduma, na tunatambua ni huduma gani pale tu tunapokuwa katika uwepo wake (Hesabu 17:8).

Hapa ndipo tunapoweza hasa kupokea ahadi za Mungu katika Neno lake. Tunapozipokea hapa, tunajua kwamba tutakuwa nazo!

Neno la Mungu katika wafilipi 4:19 linasema "Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu." Hapa unakuwa katika utukufu! Huu hapa utajiri wote wa mbinguni unakungojea.

Anza kumshukuru Mungu kwamba mambo haya matatu siyo tu kwamba yapo mbele zako, bali pia yako NDANI yako. Siyo tu kwamba yako NDANI yako lakini damu na kiti cha rehema na malaika wanakulinda kwa hayo. Katika Zaburi 91 tunasoma kwamba malaika zake watakulinda katika njia zako zote.

Sasa umeandaliwa kuwa mwombezi hasa. Unashiriki huduma ya Ukuhani Mkuu wa Yesu na kuwaombea wengine ipasavyo. Yesu alisema katika Yohana 15:7 "Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa."

Huu unapaswa kuwa muda mzuri wa kustarehe na kufurahi katika uwepo wa Mungu. Tumia muda wa kutosha hapa katika hali ya ukimya na kufurahia kuwa pamoja naye. Hupaswi hata kuongea. Mungu anafurahia jambo hili. Wewe pia utalifurahia. Jambo hili ndilo lililozungumzwa katika somo hili, yaani kuingia katika uwepo wa Mungu! Usisome tu jambo hili na kuendelea.

Amua kabisa kwamba kila siku utafanya zoezi la kuingia katika uwepo wa Mungu. Jambo hili ni muhimu sana ili kupata ushindi katika maisha haya na yale yajayo.

Kiambatisho F Kujichunguza Kiroho

Upasuaji unahitajika?

Iwapo Roho Mtakatifu anatuonyesha dhambi, tunahitaji kwenda pale ambapo Bwana alikutana nasi kwa mara ya kwanza. Ni pale msalabani. Tunamuona Yesu akiwa amesulibiwa tena, kwa ajili ya dhambi hiyo, amebeba adhabu yetu.

Damu inachuruzika chini kutoka msalabani. Hali hiyo inapaswa kutushtusha na kutuhuzunisha kwa sababu tunaona hukumu ya Mungu ya kutisha. Tunahitaji kufahamu kwamba ghadhabu yote na hukumu ya Mungu iliwekwa juu ya Yesu msalabani.

Yesu anatusubiri pale, siyo kutuhukumu, bali anafurahi tukienda msalabani na kumpa dhambi zetu. Wakristo wengi wanapotambua dhambi humkimbia Mungu kwa aibu na kujisikia hatia.

Dawa ya Mungu ya dhambi ni kwenda Msalabani, kwenda Patakatifu pa Patakatifu katika uwepo wake na kuruhusu tabia yake itawale tabia yako. Utakatifu wake utaondoa dhambi zako. Hii pekee ndiyo dawa. Hatuwezi kufanya jambo hili sisi wenyewe. Ni kanuni ya kuondoa na kuweka. Hatuondoi dhambi zetu, Mungu ndiye anayetujaza utakatifu na upendo wake na dhambi lazima iondoke. Usikate tamaa iwapo inakubidi kufanya hivi mara kwa mara. Mungu hatuhukumu.

Anayefanya hivyo ni Shetani. Mungu atakukaribisha kila wakati utakapomwendea. Ukiacha kumwendea hapo ndipo anapohuzunishw.

Tembea katika nuru ya kweli. Acha kujidanganya, ikabili dhambi hii kama ilivyo. Iache kabisa kwa moyo wa dhati. Simama upande wa Mungu na kuipinga dhambi hiyo. Kusudia moyoni mwako kutoirudia KAMWE.

Kuungama: “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.”(1 Yoh 1:9).

“BWANA amejaa huruma na neema Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili. Yeye hatateta siku zote, wala hatashika hasira yake milele. Hakututenda sawasawa na hatia zetu, wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu; maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, kadiri ile ile rehema zake ni kuu kwa wamchao. Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.” (Zaburi 103:8 12).

Msamaha siyo tu kuondoa. Msamaha ni neno zito linalomaanisha kukata na kuondoa kama daktari wa upasuaji anavyokata na kuondoa saratani. Msamaha wa dhambi unamaanisha kwamba dhambi imeondolwa kwako na kuwekwa kwa Yesu aliyeibeba msalabani.

Kuungama ni kukubaliana na jinsi Mungu anavyoliona jambo na kulitamka kwa kinywa chako. Kuungama siyo kutamka tamka tu, ni pamoja na kukubaliana na Neno. Unyenyekevu ni kukubali kwamba umekosea.

Je, utafanya hivyo sasa? Uko tayari kama mtoto mdogo kumwendea Baba yako mwenye neema na upendo na kungama dhambi zako na kuomba msamaha kwa unyenyekevu?

“Ee Mungu, unajua upumbavu wangu, wala hukufichwa dhambi yangu…kwa ajili ya jina lako, Unisamehe uovu wangu, maana ni mwingi…BWANA kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama? Lakini kwako kuna msamaha, ili Wewe uogopwe.

Ee Mungu Baba yangu, nakuja mbele zako kuungama dhambi yangu (zangu) ya (za): (Sasa zitaje na kuziungama.)

Neno lako linasema kwamba matendo haya au mwenendo huu ni dhambi nami nakubaliana na Neno lako. Sina udhuru. Sitaki tena kufanya dhambi hii ndani ya roho, nafsi na mwili wangu. Nataka kuiacha na kutupa mbali nami. Inanitenganisha mimi na wewe. Inaniharibu. Nataka kuponywa, roho, nafsi na mwili, na pia nataka kuwa karibu na wewe. Napokea msamaha wako. Asante kwa kuweka dhambi hii juu ya Yesu, na asante kwa kuwa aliiweka juu ya Msalaba wake kwa ajili yangu. Najua sistahili msamaha lakini nashukuru kwa kuniweka huru.”

Malipizo ni utayari wa kulipa au kurudisha kitu fulani kila inapowezekana. Iwapo sasa umesamehewa mbele za Bwana , uko tayari kumwomba akupe ujasiri wa kuungama na kufanya malipizo kwa wengine uliowakosea? Ukitaka kuwa huru kweli kweli dhamiri yako lazima iwe safi mbele za Mungu NA wanadamu. Huwezi kumtetea Mungu huku unajiona mchafu mbele za macho ya watu wengine.

Kumbukumbu za kushindwa kwako mbele ya macho yao zitakuingiza ndani sana katika utumwa kila wakati unapowakumbuka. Kama hujawaomba msamaha, hali ya kujihisi una hatia itaiua imani yako na kukuibia mwelekeo na nia yako. Hata hivyo, hupaswi kuungama kila dhambi kwa kila mtu; ni dhambi zile tu ulizowatendea watu unaowajua.

Kanuni: Maungamo yanapaswa kufanywa kulingana na dhambi zilizotendwa. Kama ulitenda dhambi mbele za Mungu peke yake, Mungu atakusamehe na kusahau uliyoyatenda (Zaburi 103:8-13; Isaya 43:25; Yeremia 31:34). Dhambi ulizotenda mbele za Mungu na wanadamu ni lazima uzitubu mbele za wote WAWILI, Mungu na mtu (watu) uliyemkosea (uliowakosea).

Baadhi ya yale yaliyomo katika Kiambatisho F yalichukuliwa kutoka katika vijitabu vya Winkie Pratney vilivyochapishwa katika mtandao wa kompyuta (www)